Thursday, May 12, 2016

USIJISABABISHIE KHASIRA

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

16- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa kuna mtu alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuusie ambapo akamwambia: “Usighadhibike." Yule mtu
akakariri [kuomba kuusiwa] ambapo akamwambia tena: "Usighadhibike."
Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Usighadhibike."
Bi maana usijiingize katika njia mbali mbali zinazopelekea katika khasira. 
Hivyo, kila njia miongoni mwa njia ambayo inapelekea katika kukasirika, imekatazwa kuindekeza.
 Ukiona kitu na wewe unajua fika ndani ya nafsi yako kuwa kitakupelekea katika kukasirika, Hadiyth inaonyesha kuwa ukomeke nacho tokea mwanzo na usikiendekeze na hatimaye ukakasirika na pengine ukashindwa kuzima khasira zako.

Mzungumzaji: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
Chanzo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 252-253

No comments:

Post a Comment