ASALAM ALEYKUM
Baada ya Kumshukuru Allah (سبحانه وتعالى)) na Kumtakia Rehma na Amani Mtume(صلى الله عليه وسلم) , tunapenda kuwausia kama tunavyo ziusia nafsi zetu Kumcha Allah (سبحانه وتعال) ukweli wa kumcha.
Sisi ni vijana wenye kutafuta elimu, tumeonelea kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kuwepo na tovuti hapa Tanzania ambayo itasaidizana na tovuti zingine katika kusambaza Mafundisho sahihi ya dini ya kiislam.
Mafundisho ambayo yameegemea katika QUR'AN na SUNNA kwa UFAHAMU WA WEMA WALIOTANGULIA(Manhaj Salafy).
Tovuti hii haipati misaada kutoka sehemu yoyote wala upande wowote bali ni ya kujitolea tu kwa ajili ya Allaah (سبحانه وتعالى).
Tovuti hii haiko chini ya serikali wala chama
chochote na haina mielekeo yoyote ya kisiasa, mapote potevu wala fikra
za kisiasa.
Ama kuhusu usambazaji wa chochote kilichomo kwenye
www.nadhiru.blogspot.com, haihitaji mtu kupewa idhini kwa kuchukua chochote
ndani ya tovuti hii kikatumiwa kwa lengo la kueneza Da'wah kwa watu.
NB:
- Unaruhusiwa kunakili na kusambaza kile kinachopatikana humu BILAKUBADILISHA CHOCHOTE !!
- Endapo kuna Mapungufu yoyote katika uendeshaji wa tovuti hii TUMA UJUMBE WAKO KATIKA UKURASA WA KWANZA CHINI KUSHOTO. Kwani binadamu hukosea na Ukamilifu ni wa ALLAH ( سبحانه وتعالى)
BARAKA LLAHU FYKUM
No comments:
Post a Comment