KUFUKIZA UBANI
WAKATI WA KUOMBA DUA
بسم الله الرحمن الرحيم
إن الحمد لله، نحمده ونستعينه،
ونستغفره، ونعوذ بالله من شرور أنفسنا، وسيئات أعمالنا، من يهده الله فلا مضل له،
ومن يضلل فلا هادي له، وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمدا
عبده ورسوله.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا
اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ] آل عمران:102 [يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا
رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا
وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ
وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ
اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا] النساء:1 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا
اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾ يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ
وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن
يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا . الأحزاب:70-71
Sifa zote
njema anastahiki Allah aliyetukuka Mola mlezi wa walimwengu wote, swala na salamu
zimshukie Kipenzi chetu mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم:) na maswahaba
zake mpaka siku ya mwisho.
KUFAA KUTAJA MABAYA KWA LENGO LA TAHADHARI, NA HASA KTK DINI.
Amesema Imaam Muslimرحمه الله تعالى ktk
utangulizi wa: Sahiyh yake:
[وَإِنَّمَا
أَلْزَمُوا أَنْفُسَهُمْ الْكَشْفَ عَنْ مَعَايِبِ رُوَاةِ الْحَدِيثِ وَنَاقِلِي
الْأَخْبَارِ وَأَفْتَوْا بِذَلِكَ حِينَ سُئِلُوا لِمَا فِيهِ مِنْ عَظِيمِ
الْخَطَرِ. إِذْ الْأَخْبَارُ فِي أَمْرِ الدِّينِ إِنَّمَا تَأْتِي بِتَحْلِيلٍ
أَوْ تَحْرِيمٍ أَوْ أَمْرٍ أَوْ نَهْيٍ أَوْ تَرْغِيبٍ أَوْ تَرْهِيبٍ فَإِذَا
كَانَ الرَّاوِي لَهَا لَيْسَ بِمَعْدِنٍ لِلصِّدْقِ وَالْأَمَانَةِ ثُمَّ
أَقْدَمَ عَلَى الرِّوَايَةِ عَنْهُ مَنْ قَدْ عَرَفَهُ وَلَمْ يُبَيِّنْ مَا
فِيهِ لِغَيْرِهِ مِمَّنْ جَهِلَ مَعْرِفَتَهُ كَانَ آثِمًا بِفِعْلِهِ ذَلِكَ
غَاشًّا لِعَوَام الْمُسْلِمِينَ]
[Na kwa hakika si vinginevyo, Wanachuoni walizilazimisha nafsi zao, kwa
kuziweka wazi na kuzifunua aibu za wapokezi wa hadithi na wale wenye kunukuu
khabari, na wakatoa fatawa juu ya kufaa kwa hilo pale walipoulizwa. Hilo
walilifanya kutokana na kuwa jambo hili la kutowaelezea wapokezi wenye kasoro lina
hatari kubwa, kwa sababu khabari zinazohusiana na mambo ya dini huwa zinakuja
ima kwa kuhalalisha au kuharamisha, au kuamrisha au kukataza, au kupendezesha
jambo fulani, au kutishia jambo hilo. Basi pindi atakapo kuwa mpokezi wa
khabari hizo sio mtu wa kujipamba na ukweli na uaminifu, kisha akazitanguliza
riwaya au khabari hizo kutoka kwake kwenda kwa yule ambae anamjua, na akawa
hakubainisha yale ambayo yapo ktk riwaya hiyo au khabari hiyo –kutokana na udhifu
wa khabari hiyokwa yule asiejua khabari hiyo kama ni dhaifu, kufanya kwake
hivyo atakuwa amepata madhambi kwa kitendo chake hicho, na atakuwa amewafanyia
ghishi wale Waislamu wasio jua]
KWA NINI TUNATOA NASAHA
عن أبي
رُقَيَّةَ تَمِيمِ بنِ أوْسٍ الدَّارِيِّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ النَّبي صلى الله
عليه وسلم قالَ:((الدِّينُ النَّصِيحَةُ)). قُلْنَا: لِمَنْ ؟ قالَ: ((للهِ،
ولِكِتَابِهِ، ولِرَسُولِهِ، ولِلأَئِمةِ المُسْلِمِينَ، وعامَّتِهِمْ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abu
Ruqayyah Tamim Ibn Aus Addarryرضي
الله عنه ambaye amesema kuwa Bwana Mtume صلى
الله عليه وسلم kasema:
Dini ni nasaha.
Tukauliza: Kwa nani? Akasema kwa Allaah (Kukiri Uungu wake na kwamba Hana
mshirika), Kitabu chake (Kukubali kuwa ni maneno ya Allah yasiyo na shaka), na
Mtume wake (Kumkubali na kukubali ujumbe aliotumwa nao), na kwa Viongozi wa
Waislamu (Kuwatii na kuwafuata katika mema na kuwaasa katika yale wanayokwenda
nayo kinyume), na watu wa kawaida (kuusiana mema na kukatazana mabaya kwa njia
nzuri).
Imesimuliwa na Muslim
Huu ni
ukumbusho ewe ndugu yangu muislamu, na ukumbusho humfaa yule mwenye kuzingatia.
Ujumbe huu unahusu Je, kuomba dua kwa kutumia ubani ni katika sunna au ni bid’aa?
Majibu ya swali hili ni haya.
Anasema
Allah (سبحانه وتعال ) “Na
mola wenu anasema: niombeni nitawajibu, kwa hakika wale ambao wanajivuna na
kuniabudu mimi wataingia Jahannam wadhalilika” (Ghaafir:60).
Pia
kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr ( عنها رضى
الله) Mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم:) amesema “DUA
NI IBADA” . (Sunan At-tirmidhy).
Hivyo
hakuna anayepinga swala la kuomba dua
ila inatupasa tuombe kwa kufuata njia iliyo sahihi kama tulivyo pata mafunzo
Kutoka kwa Mtume Muhammad (صلى
الله عليه وسلم:) . Suala la
kuomba dua kwa kufukiza ubani katika moto wakati wa kuomba dua ni katika bid’a
na haina uhalali , wala faida yoyote na hii imekuwa ni ada kwa ndugu zetu hasa
wanaosoma Maulidi na Khitima kwa kuamini kwao kuwa dua’a inapanda juu na moshi
wake kama wasemavyo wazushi.
Yote haya
ni mambo ya Kijahili(mambo ya kijinga) yasiyokubalika katika sheria ya
kiislamu. Allah سبحانه
وتعال anasema “Fuateni
mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu” (Al-A’raf :3). Hivyo ni waajib
kufuata yale yaliyo teremshwa kutoka kwa Allah na yale aliyotufunza Mtume wetu
Muhammad (صلى
الله عليه وسلم:) kwa kufuata muongozo ulio sahihi wa
mafundisho yake. Pia katika hadiyth sahih Muslim:-
عن أُمِّ المُؤمِنينَ أُمِّ عَبْدِ الله عائِشَةَ
رَضي اللهُ عنها قالَتْ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ أَحْدَثَ
في أَمْرِنا هذا ما لَيْسَ منهُ فَهُوَ رَد))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
وَمُسْلِمٌ وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ
((مَن عَمِلَ عَمَلاً لَيْسَ عَلَيْهِ
أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ )).
Kutoka kwa Mama wa
Waislamu Ummu Abdallah ‘Aisha رضى
الله عنها ambaye alisema: Mtume wa Allaah سبحانه
وتعالى
kasema:
Yule anayezua kitu
kisichokuwemo (kisichokuwa) katika jambo (DINI) hili letu kitakataliwa .
Imesimuliwa na
Al-Bukhari na Muslim. Na katika usimulizi mwengine wa Muslim inasema hivi:
Yule anayetenda
kitendo ambacho hakikubaliani na jambo letu kitakataliwa.
Amesema
Abdullah Ibn Mas’uud (رَضي
اللهُ عنها). “Fuateni wala msizushe kwa hakika mmetoshelezwa” Hivyo jambo hili la
kuomba dua kwa ubani ni katika mambo ambayo hayajafundishwa katika uislamu.
Isipokuwa ni uzushi uliozushwana watu , na huku ni kwenda kinyume na sunna za Mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم:) .
Na kuomba
dua kwa kutumia chotezo la moto na ubani hili limechukuliwa kutoka kwa Mafursi (Iran) ambao walikuwa
wana abudu “jua” na “moto”.
Mafursi walipoingia
katika Uislamu waliingia na baadhi ya desturi zao mbaya zinazokwenda kinyume na uislamu na Mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم:) ametusisitiza
sana tusifuate desturi za makafiri na kujifananisha nao.
Mtume
Muhammad (صلى
الله عليه وسلم:) amesema “Hakika yule atakayeishi katika nyinyi basi atakuja kuona tofauti
nyingi , hivyo basi jilazimisheni na sunna zangu na sunna za Makhalifa wangu
waongofu wenye kuongoza , ziumeni sunna hizo kwa magego yenu, tahadharini na
mambo ya kuzua Hakika kila Bid’aa ni upotofu.”(Sunan Abu-Daud:3607)
Hivyo
matendo yote yanayokwenda kinyume na
sunna ni Bid’aa na kwamba kila Bid’aa ni upotovu na kila upotovu ni Motoni.
Tuna wauliza wale wenye kuomba dua kwa ubani mafundisho haya wana fundishwa na
nani? Kwa sababu Mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم:)
hakulifundisha hili na wala maswahaba hawakulifanya hili.
Na kila
kheri basi inapatikana katika karne tatu (3) bora kama alivyo alivyosema Mtume
Muhammad (صلى
الله عليه وسلم:) na kila shari
inapatikana katika mambo ya uzushi, hivyo utaratibu huu si dini bali ni uzushi
katika dini ya Allah.
Allah
anasema “Enyi mlio amini mtiini Allah na
Mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi . Mkizozana katika jambo basi
lirudisheni kwa Allah na Mtume wake mkiwa muna muamini Allah na siku ya mwisho.
Hivyo ni njia bora na matokeo mazuri zaidi” (04:59).
Kurejesha
kwa Allah ni kurejesha katika Qur’an
na kurejesha kwa mtume (صلى
الله عليه وسلم:) ni kurejesha
katika sunna zake .
Amesema
Swahaba Hudheyfah(رَضي
اللهُ عنها) Kila
ibada ambayo haikufanywa na maswahaba wa Mtume (صلى الله عليه وسلم:) basi usi
ifanye ibada hiyo kwa kuwa wale wa mwanzo hawakuacha chochote kwa wamwisho la
kuseema, Mche Allah enyi kongamano la
wasomi (Abuu Daud:7064)
Amesema
Mtume Muhammad (صلى
الله عليه وسلم:) ”Uislamu ulianza ukiwa ngeni na utarejea
kuwa mgeni kama ulivyoanza, pongezi kwa wageni” (Muslim:541) hii ndiyo hali ya sasa kwa wale wanao lingania
watu katika usawa, wanaonekana kuwa ni wageni na kutolea hoja zao “mbona jambo hilohilo mimi sikulijua na
mbona wazee wetu walikuwa wakilifanya hili”
Ewe ndugu
yangu muislamu Mche Allah, TAHADHARI! kisha TAHADHARI! na kila uzushi
katika dini na kukaa na watu wa uzushi.
Amesema
Allah (سبحانه
وتعال ) “Pindi utakapo waona wale ambao wanafuata mambo yenye utata basi hao
ndiyo hao Allah aliowasema basi tahadhari nao” (Al-Annisaa:41)
Tunamuomba
Allah (سبحانه
وتعال ) aturuzuku kushikamana na Qur’an na Sunna kwa Ufahamu wa
wema waliotangulia Mpaka siku tutayo kutana nae.
Imekusanywa na
kupangiliwa na
Abu Ayman Sai’d
bin Hassan
Tahaqiq
Abuu Khayrat
Nadhiru bin Raia
No comments:
Post a Comment