بِسمِ ٱلله الرَّحْمٰنِ الرَّحِيـمِ.
الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على رسول الله خاتم النبيين، وعلى آله وصحبه، ومن والاه إلى يوم الدين.
Ama baada ya kumhimidi Allah na kumtakia sala
na salam mtume صلى الله عليه وسلم . Yapaswa utambue kuwa, hakika Allah
tabaaraka wata’la aliumba kila kitu katika jinsi mbili na akamuumba mwanadamu
katika jinsia hizo [mume na mke] kutokana na tone la manii baada ya kumuumba
Adam kwa udongo uliovunda. Hakika zama zimepita na hakuna tofauti katika
mwenendo wa Allah tabaaraka wata’la juu ya viumbe wake. Kwani ilipokuwa nafasi
ya mwanadamu ni ya juu katika dini kuanzia mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, Allah
tabaaraka wata’la aliusia utekelezaji wa maamrisho yake kwa wanaadamu na
akawausia wanawake pia. Na alikua Mtume صلى الله عليه وسلم akiwausia
kwa miongozo hiyo kwenye hotuba katika viwanja vya Arafat
, na sehemu mbalimbali. Kwalo, ni miongoni mwa yanayo ashiria uwajibu wa kutilia umuhimu kuwakumbusha wanawake katika kila zama, na hasa hasa katika zama hizi ambazo mwanamke wa kiislamu hupigwa vita ili kumporomosh na kumuondosha katika nafasi yake na cheo chake alichopewa na Allah tabaaraka wata’la. Kwa hili, kukawa hakuna budi katika kukumbushana na kutanabahisha khatari inayowakabili wanawake wengi katika zama hizi katika mama zetu na dada zetu na kutaja yale yenye manufaa kwao na sifa ya njia ya mafanikio huenda Allah tabaaraka wata’la kwa tawfiq yake akazifungua nyoyo zilizolala.
, na sehemu mbalimbali. Kwalo, ni miongoni mwa yanayo ashiria uwajibu wa kutilia umuhimu kuwakumbusha wanawake katika kila zama, na hasa hasa katika zama hizi ambazo mwanamke wa kiislamu hupigwa vita ili kumporomosh na kumuondosha katika nafasi yake na cheo chake alichopewa na Allah tabaaraka wata’la. Kwa hili, kukawa hakuna budi katika kukumbushana na kutanabahisha khatari inayowakabili wanawake wengi katika zama hizi katika mama zetu na dada zetu na kutaja yale yenye manufaa kwao na sifa ya njia ya mafanikio huenda Allah tabaaraka wata’la kwa tawfiq yake akazifungua nyoyo zilizolala.
KUHUSU MWILI
[MAUMBILE] KWA UJUMLA
Fahamu kuwa;
1.
Ni haramu
kunyoa au kupunguza nyusi kwa njia yeyote ile ila itakapokuwa hakuna budi
kufanya hivyo kwa sababu kunyoa nyusi ni kubadilisha maumbile ya Allah
tabaaraka wata’la.
Anasema mtume
صلى الله عليه وسلم :
لعن (صل الله عليه و سلم) النامصة والمتنصة
Na akasema
pia صلى الله عليه وسلم :
لعن الله الواشمات و المستوشمات و النامصات و المتنمصات و المتفلجات للحسن المغيرات خلق الله عز و جل
“Allah
Amemlaani al-waashimaat na mustawshimaat na an-naamiswaat na al-mutanamiswaat
na al-mutafaljaat kwa ajili ya urembo wenyekubadilisha umbile la Allah Mshindi,
Mtukufu.”
Na wala haifai kwa mwanamke kumtii mumewe
atakapo muamrisha kufanya hivyo , kwa hakika kufany hivyo ni kumuasi Allah
tabaaraka wata’la.
Fahamu kuwa;
2.
Na niharamu
kwa mwanamke wa kiislamu kunyoa nywele zake zote au kupunguza baadhi yake bila
ya dharura ya kisheria na ikiwa anakusudia urembo au kujifananisha na wanawake
wa kisasa.
Amesema mtume
صلى الله عليه وسلم :
ليس على النساء حلق اِنما على النساء التقصير
Si
haki kwa mwanamke kunyoa nywele, hakika hapana vingine isipokuwa ni kupunguza
tu[3]
Na wamesema wanachuoni; kauli yake (Mtume) katika kuzuiwa kunyoa mwanamke kichwa chake “kwani hakika nywele ndefu za wanawake ni
kama ndevu kwa wanaume katika muonekano na uzuri . . .[4]
Ama
ikiwa kupunguza nywele za
kichwa chake ikiwa ni kwa haja isiyokuwa kujipamba kama vile kushindwa
kuzitunza au zinarefuka sana na zinampa shida hakuna ubaya katika hili na iwe
kwa kiasi cha haja na wala asiziondoe zote. Kama walivyokuwa wake wa Mtume
(Swallallahu Alayhi Wasallam) wakifanya baada ya kufa kwake kwa ajili ya
kuwacha kujipamba baada ya kufa kwake mtume.[5]
Basi ni juu ya mwanamke kuzihifadhi nywele za
kichwa chake na kuziweka mafungu mafungu[6].
Na haifai kwa mwanamke kuzikusanya juu ya kichwa au kuzielekeza kichogoni kama
wafanyavyo wengi katika wanawake, bali wengine huweka vibanio ili
kujipendezesha na yote haya ni katika mabaya yenye kuchukiza.
Amesema sheikhul-islami ibin tyimiyyahallah
amrehemu kuwa “kama walivyokusudia
baadhi ya wanawake makahaba kuziweka nywele fungu moja zikiwa ni zenye kupenya
baina ya mabega mawili.”[7]
Na amesema sheikh Muhammad bin Ibrahim: “Na ama wanayofanya wanawake wa kiislamu
zama zetu hizi katika kuzigawanya pembeni nywele za kichwa na kuzikusanya
upande wa kichogoni au kuzijaalia juu ya kichwa kama wanavyofanya wanawake wa
kizungu, basi hili halifai kwasababu ya kujifananisha na wanawake makafiri.
Kwani;
Amesema Mtume wa
Allah صلى الله عليه وسلم :
“namna
mbili ni miongoni mwa watu wa motoni sijapatapo waona namna hizo – watu wenye
fimbo kama mikia ya ng’ombe wanapiga watu kwa fimbo hizo; na wanawake
wenyekuvaa (lakini bado) wapo uchi; wenyekutembea kwa maringo na wanahimiza
watu watembee kwa maringo; na vichwa vyao ni kama nundu za ngamia wenye
kukonda. Hawatoingia Jannah na wala hawatopata harafu yake, basi hakika harufu
yake inapatikana katika masafa kadha wa kadha”[8]
Na hakika wamefasiri
baadhi ya wanachuoni kuwa wao wanasuka nywele zao mtindo wa “Maila” nao
ni mtindo wa wanawake makahaba.
Na inaruhusiwa kupunguza kwa ibada ya hijjah
kiasi cha ‘unmilah’. Akisema Ibn Qudamah (Allah amrehemu):
“Na jambo la sheria kwa mwanamke ni kupunguza
kinyume na kunyoa. Hakuna tofauti (ikhtilafu) katika hili”[9]
Fahamu
kuwa;
3.
Ni haramu kuziunga au kuzidisha juu yake
nywele za mwengine (kuweka rasta au kuzichoma). Nayo ni hukmu ya jumla kwa
mwenye kufanyia na mwenye kuwafanyia wenzake kwani;
Amesema mtume صلى الله عليه وسلم :
لعن رسول الله (صل الله عليه و سلم) الواصلة و المستوصلة.
“Amemlaani Mtume wa Allah
(Swallallahu Alayhi Wasallam) mwenyekuunganisha na mwenyekuunganishwa”[10]
Na imesimuliwa pia:
Alitoa hotuba wakati
alipofika Madina na akatoa kofia la nywele au kifurushi cha nywele kisha
akasema: wana nini wake zenu?! , Wanajaalia katika vichwa vyao mfano wa hili?
Nimemsikia Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) anasema “haiwi kwa mwanamke
yeyote anaye weka kwenye kichwa chake nywele za mwengine ispokuwa huwa ni
udanganyifu (kwa kutumia urembo bandia).”[11]
Fahamu kuwa;
4.
Ni haramu kwa mwanamke wa kiislamu kuachanisha
meno yake na kuyachonga kwa tupa mpaka ukatokea kati ya meno yake mwanya mdogo
kwa tamaa ya kujiremba.
5.
Ni haramu kwa
mwanamke kupaka rangi za kucha ambazo zitazuia maji kufika katika kucha wakati
wa kutawadha kama ambavyo haifai kupaka katika sehemu nyingine za mwili kama
vile mashavu nk.
Bali
kilichosawa kwake ni kupaka HINA
kama ilivyonukuliwa kwa mama ‘Aisha allah amuwie radhi:
“hakika mwanamke Fulani alimuliza Aisha (Allah amuwie radhi) kuhusu kupaka hina. Na
alisema Aisha: “hakuna ubaya, lakini mimi ninaichukia. Kwa sababu kipenzi
changu Mtume wa Allah (Swallallahu Alayhi Wasallam) alikuwa inamchukiza harufu
yake.”[12]
Na akasema mtume صلى الله عليه وسلم
:
ما
أدري أيد رجل أم يد امرأة ؟ قالت : بل يد
امرأة : قال : لو كانت امرأة لغيرت أظفارك. – يعني بالحنا
“sijui ni mkono wa mwanamme au ni wa
mwanamke?” alijibu yule mwanamke “bali ni wa mwanamke”: akasema (Swallallahu
Alayhi Wasallam) “lau ungelikuwa ni wa mwanmke zingelibadilika kucha zako” akikusudia
kwa kupakwa hina.”[13]
6.
Haifai kwa mwanamke (kadhalika mwanaume) kupaka
rangi nywele zake, ikiwa ni mvi basi hakika yeye atazipaka kwa rangi isiyo
nyeusi kwani, kupaka rangi nyeusi ni jambo lisilofaa.
Kwa sababu ya ujumla wa makatazo yake (صلى الله عليه وسلم)
kuhusu kupaka nywele kwa rangi nyeusi.
Kama alivyosema Imam An-nawawy katika Riyadhi Swalihina katika mlango wa ‘makatazo
ya mwanamke na mwanamme kuhusu kupaka nywele zao kwa rangi nyeusi’.
Ziada:
Yafaa kwa mwanamke kujipamba kutokana na dhahabu na fedha mapambo
ambayo yamezoeleka kama bangili na hereni.
Lakini haifai kwa mwanamke kuonyesha mapambo hayo kwa wanaume
wanaoweza kumuoa, bali ayafiche hasusan wakati wa kutoka nyumbani na kwenye
msongamano wa macho ya wanaume, na ashushe sauti yake mbele yao.
KATIKA MAVAZI
Fahamu kuwa;
1.
Hakika yapasa vazi la mwanamke wa kiislamu liwe
zito linalositiri mwili wote ili kuepukana na wanaume wanaoweza kumuoa na
hakuna ubaya kupunguza stara kwa wale ambao ni haramu kumuoa na wanawake wenzake. Pia, liwe ni lenye kusitiri
ambacho kipo ndani yake, wala lisiwe jepesi (mpaka) inaonekana kutoka ndani
yake rangi ya ngozi yake au likabana na likaonesha viungo vyake.
2.
Haifai kujifananisha katika mavazi na wanaume.
kwani amelaani Mtume صلى الله عليه وسلم
mwanamke mwenye kujifananiza na mwanaume.
3.
Haifai vazi la mwanamke kuwa na mapambo
(ambayo yanashawishi) macho (ya watu) kumuelekea wakati wa kutoka nyumbani
kwake.
4.
Ni wajibu kwa mwanamke wa kiislam kuvaa juba
ambalo litafunika kuanzia kichwani mwake (pamoja na uso wake) mpaka chini.
Kwani imepokelewa kutoka kwa Mama ‘Aisha allah
amuwie radhi:
كان الركبان يمرون بنا و نحن مع رسول الله صلى الله عليه و سلم محرمات فاِذا حاذوا بنا سدلت اِحدانا جلبابها من رأسها على وجهها فاِذا جاوزنا كشفناه
“Walikuwa wapanda farasi
wakitupitia na sisi tupo pamoja na Mtume wa Allah (Swalla Allahu Alayhi Wa
Sallam) ni wenye kuvaa mavazi ya Ihramu, pindi wanapoelekea kwetu anaachilia
mmoja wetu hijabu yake kutoka kichwani kwake juu ya uso wake , na wakitupita
tunazifunua”[14]
Na amesema sheikhul-Islamu Ibin
Taymiyyah (Allah Amrehemu):
“na hijabu nayo ni vazi lenye kuenea mwilini,
nalo ndio ambalo huliita Ibin Mas’ud na mwenzake mtandio na unaweza
kuliita ni shuka kubwa. Nayo ni shuka kubwa ambayo hufunika kichwa chake
(mwanamke) na sehemu nyengine ya mwili wake. Na hakika alisimulia Abu Ubaidah
na mwenzake “hakika yeye (mwanamke) huishusha kutoka juu ya kichwa chake na
haonyeshi ispokuwa macho yake na miongoni mwa jinsi yake ni niqabu……”[15]
KATIKA MSIBA
Fahamu
kuwa;
1.
Amekataza Allah tabaaraka wata’la kufanya
maombolezo katika msiba kwa kunyanyua sauti na kupasua nguo, kujipiga makofi,
na kung’oa nywele na kujipaka masinzi usoni na kwa ajili ya kuhuzunika juu ya
maiti na dua za majuto na mfano wa hayo yenye kuononesha kuhuzunika kwa ajili
ya hukumu ya Allaha na makadirio yake na kukosa subira, kwani;
Amesema
mtume صلى الله عليه وسلم :
ليس منا من لطم الخدوه و شق الجيوب و دعا بدعوى الجاهلية
Si katika sisi mweny kupiga makofi
mashavu yake na kupasua magauni, na kuomba dua za jaahiliyyah (ujinga).
Na akasema pia صلى الله عليه وسلم
:
برىء من الصالقة و الحالقة و الشاقة
Amejitenga mwenye kufanya ‘mwenye kunyanyua sauti yake wakati wa msiba’ na ‘mwenye kunyoa nywele zake wakati wa msiba’ na ‘mwenye kupasua nguo zake wakati
wa msiba’[16]
Na akasema pia صلى الله عليه وسلم :
لعن النائحة و المستمعة
Amemlaani mwenye kutoa sauti kuomboleza
na msikilizaji[17]
NASAHA ZA JUMLA
Fahamu kuwa;
1.
Ni haramu kwa mwanamke kuwapa mikono wanaume
wanaoweza kumuoa hata kwa kuweka kitambaa,kanga na mfano wa hivyo katika mkono
wake kama wafanyavyo wengi[MAHARIM kwake].
2.
Haifai
kuwalaani watoto wadogo na wasiokuwa hao kama wafanyavyo wengi katika wazazi
watoto wao wanapokosea.
3.
Ni wajibu
[lazima] mwanamke asome dini ya Allah, afanyie kazi, na awafundishe wanawake
wenzake na watoto wadogo wa familia yake.
4.
Kwa hakika
mwanamke atakaposwali, akafunga, akajihifadhi na akawa mtiifu basi ataingia
katika Jannah ya Allah katika mlango autakao. Amesema mtume صلى الله عليه وسلم :
HITIMISHO
قُلْ
لِلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ذَلِكَ
أَزْكَى لَهُمْ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ (30) وَقُلْ
لِلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا
يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ
عَلَى جُيُوبِهِنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ
آَبَائِهِنَّ أَوْ آَبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ
بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي
أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ
التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ
الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَى عَوْرَاتِ النِّسَاءِ وَلَا يَضْرِبْنَ
بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِنْ زِينَتِهِنَّ وَتُوبُوا إِلَى
اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ (31)
30. “Waambie Waumini
wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao.
Hakika Allah anazo khabari za wanayo yafanya”.
31. “Na waambie Waumini
wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasioneshe uzuri wao
isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala
wasioneshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au
watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana
wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume
[waliowalea], au wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo
yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo
yaficha. Na tubuni nyote kwa Allah, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa”[18]
Hizi ni dondoo zilizofupi nasaha [maalum]
kwa MAMA,NDUGU ZANGU WA KIKE na [jumla] kwa mwengine atakayesoma risala hii.
Namuomba ALLAH anisamehe nilipokosea na anilipe kwa lile nililopatia na
atuafikishe mimi na mama yangu na watu wote katika kheri yake. Hakika hakuna
mkamilifu isipokuwa Allah.
Makala hii Imeandaliwa na
ABU KHAYRAT
Nadhiru Ngozi
وصلى الله وسلم على نبينا محمد وعلى آله
وصحبه أجمعين
[1]
Maana ya an-naamiswat ni mwanamke ambaye hukata nyusi zake.
[2]
Maana ya mutanammiswat ni mwanamke mwenye kutata au kukatiwa nyusi.
[3]
Abu dawud
[4]
Taz: Majmuu’l_fatawa ya sheikh Muhammad Ibrahim 49/2 akinukuu Mirqaat sherh ya Al-mishkaat
[5]
Sheikh fawzani katika kitabu chake alichokiita: TANBIHI JUU YA HUKUMU ZA KISHERIA ZINAZOHUSU WAUMINI
WANAWAKE. na akasema: Na ama ikiwa kusudio la mwanamke
katika kuzipunguza nywele zake ni kujifananisha
na makafiri wa kike na waovu wa kike au
kujifananisha na wanaume basi hilo ni haram bila shaka.
[6]
Kuzisuka
[7]
Majmuul-fatawa
(22/145)
[8]
Imam Muslim
[9]
Kitabu: Al-mughniy.
Faida: Amesema Ibin Mundhir; “wamekubaliana maulamaa kwenye jambo
hili na hivyo ni kwa
sababu kunyoa katika haki yao wanawake ni
kuchupa mipaka. Kama hivi wamepita Ibn ‘Umar, Imam_shafi’ nk.
[10]
Bukhari na Muslim
[11]
Bukhari na Muslim
[12]
Abu Dawud
[13]
An-nasai na Abu Dawud
[14]
Abu Dawud, Imam Ahmad na Ibn Majah. (Na hii pia ni dalili ya uvaaji wa niqab
kwa mwanamke).
[15]
Majmuu’l_fatawa
[16]
Bukhari na Muslim
[17]
Muslim
[18]
Surattn_nuur
No comments:
Post a Comment