Msimamo Kwa Wanawachuoni WAZUSHI
Imaam Ibn Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
"Hali kadhalika mzushi yuko dhidi ya Sunniy kwa sababu anamfuata
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na halinganishi Sunnah na maoni
ya wanaume wala na kitu kingine kinachoenda kinyume nayo."
Ukimwambia mzushi: "Mche Allaah! Hii ni Bid´ah. Shikamana na Sunnah",
anasema: "Mambo haya yana tofauti." Hivi kweli kuna tofauti katika
kushikamana na Sunnah? Ndio, kwao kuna tofauti. Wanasema: "Lau ingekuwa
wajibu kushikamana na Sunnah basi mwanachuoni fulani na fulani
wasingeenda kinyume." Katika wazushi kuna wanachuoni, lakini maoni yao
yanachukuliwa?
Hapana, hayachukuliwi. Haijalishi kitu hata kama ni
wanachuoni.
Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (20)
http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighasah-12-2-1435-01.mp3
Toleo la: 16.04.2016
No comments:
Post a Comment