Saturday, May 14, 2016

INAFAA KUNYANYUA MIKONO WAKATI WA KUOMBA DUA?

Swali
Ni ipi hukumu ya kuomba Du´aa katika vikao vya elimu na kunyanyua mikono miwili na wasikilizaji kuitikia “Aamiyn”?

Jibu
Du´aa na kunyanyua mikono ni mambo yanayotakikana
Hakuna neno kwa hayo. Atakapoomba Du´aa mwalimu na akanyanyua mikono na wengine watanyanyua mikono yao na kuitikia “Aamiyn” kwa Du´aa yake. 
Hakuna neno juu ya hilo. 
Kwa kuwa asli ni kunyanyua mikono isipokuwa sehemu ambazo imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba na hakunyanyua mikono yake. 
Kwa mfano wa Khutbah siku ya Ijumaa, Du´aa katika Swalah isipokuwa katika Qunuut ya Witr.
 
Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

No comments:

Post a Comment