عن أبي هُرَيْرَةَ رضي اللهُ عنه أنَّ
رَجُلاً قال لِلنَّبِّي صلى الله عليه وسلم: أَوصِني، قالَ:
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
16- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa kuna mtu alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuusie ambapo akamwambia: “Usighadhibike." Yule mtu akakariri [kuomba kuusiwa] ambapo akamwambia tena: "Usighadhibike."
Imepokelewa katika Sunnah Hadiyth nyingi kuhusiana na jinsi ya kutibu khasira. Tunazikusanya ifuatavyo:
- Khasira inatibiwa kwa Wudhuu. Mwenye kukasirika ni jambo limewekwa katika Shari´ah akatawadha.
- Akikasirika na hali ya kuwa amesimama anatakiwa kukaa. Huku ni katika kutibu athari za khasira. Kwa kuwa huituliza nafsi yake.
- Ajitahidi kujizuia na badala yake alete maneno ambayo ni mazuri. Hili linamuhusu yule anayeweza kufanya hivo.
Chanzo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 254
No comments:
Post a Comment