Usidanganyike
na yule anayemsifu mtu kama huyu na kumtapa.
Watu wapotevu wanaweza
kuwa na kitu katika wema, lakini unachotakiwa kutazama ni ule upotevu
walionao.
Usidanganyike na kitu kidogo katika kheri na ukasahau yale
mambo mengi ya shari [waliyomo].
Hii ni hekima kubwa.
Baadhi ya
watu wanasema “Fulani ana kheri hata kama ni mpotevu”, “Fulani ni
mkarimu na kadhalika”.
Achana na yote haya!
Maadamu ni mtu wa upotevu na
ni mtu anafuata matamanio yake, achana naye hata kama ana kitu katika
kheri. Achana naye.
Mtu wa Sunnah hata kama atakuwa na maovu na maasi, shikamana naye kwa kuwa ni mtu ameshikamana na Sunanh.
Chanzo: https://www.youtube.com/watch?v=KNvT1bMto4U
Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
No comments:
Post a Comment