Sunday, May 15, 2016

HARAMU HAITOLEWI SWADAQAH

Swali
Inajuzu kuwapa makafiri mafukara kondoo aliyekufa mwenyewe?

Jibu
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ
"Enyi mlioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambayo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa na hali nyinyi wenyewe si wenye kuvichukuwa isipokuwa kwa kuvifumbia macho." (02:267)


Hiki si kwamba ni kichafu tu, bali ni haramu
Hiki si kwamba ni kibaya tu, bali ni haramu. 
Haijuzu kutoa swadaqah kwa kitu haramu, si kumpa kafiri wala muislamu.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah--14340316.mp3

No comments:

Post a Comment