Monday, May 9, 2016

JE, INAJUZU KUMPA SALAMU AU KUPOKEA SALAMU YA KAFIRI?

Swali la Kwanza:
Inajuzu kuanza kuwapa Mayahudi na Manaswara Salaam (kuwasalimia)?


Jibu
Jibu ni kuwa HAIJUZU
Kakataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuanza kuwasalimia.

Swali La Pili:
Na vipi ikiwa wataanza kutusalimia, je tuwaitikie?

´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu tunasema kama ilivyokuja katika Hadiyth. Wakiwasalimia Mayahudi na Manaswara mjibu "wa ´alaykum." 

Wakisema "as-Saam´alaykum", na maana ya as-Saam ni mauti, wanabadilisha maneno, yaani wanawatakia mauti kwa kutumia Salaam. 
Wakisema "as-Saam ´alaykum" (mauti yawe juu yenu), nanyi mseme "wa ´alaykum" (nanyi pia).

Akikuchezea shere hukusikia vizuri kama amesema as-Saam au amesema as-Salaam, watakiwa useme "wa ´alayka". 
Mtu huchukulia asli. Ama akikusalimia kwa ibara ya wazi kabisa, akisema "as-Salaam ´alaykum", wewe useme "wa ´alaykum-us-Salaam".
”Allaah Hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Allaah huwapendawafanyao uadilifu.” (60:08)
Akikwambia "as-Salaam ´alaykum", mjibu umwambie "wa ´alaykum-us-Salaam". 
Na hii ndo Fatwa wataoyo wanachuoni.

´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy

No comments:

Post a Comment