Wednesday, May 11, 2016

IBADA MAALUMU USIKU WA NISFU SHA 'BAAN NI BID 'AH

Swali:
Hadiyth zilizopokelewa kuhusu fadhila za usiku wa Nifsu Sha´abaan ni Swahiyh?
Jibu
Hapana. Sio Swahiyh
Hakukusihi kitu juu ya usiku wa Nisfu Sha´abaan wala siku ya Nisfu Sha´abaan. Mtu asisimame usiku wa Nisfu Sha´abaan, bi maana mtu asikhusishe kusimama usiku.
Ama kuhusu yule aliyekuwa akidumu kwa kusimama tokea mwanzo asimame usiku wa Nisfu Sha´abaan kama siku zingine. Ama kusema aikhusishe kwa kusimama, hii ni Bid´ah
Au akafunga siku ya kumi na tano ya mwezi wa Sha´abaan, hii ni Bid´ah
Isipokuwa yule aliyekutwa akifunga Swawm zake kama kwa mfano Swawm ya masiku meupe, afunge katika Sha´abaan na siku zingine.

Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

No comments:

Post a Comment