Saturday, May 14, 2016

MTU AKITOKA KISHA AKARUDI KWENYE KITANDA CHAKE ASOME ADHKAAR UPYA ?

Swali
Nikisoma Adhkaar za kulala halafu nikashegama, kisha nikaenda kukidhi haja kwa kusahau, kisha nikarudi kwenye kitanda mara ya pili na wala hapakupita muda mrefu.
 Je, nirudie kusoma Adhkaar mara nyingine?

Jibu
Hapana. Inatosha kusoma kwake mara ya kwanza. 
Kwa kuwa ulienda kwa haja na ukarudi. 
Wewe una hukumu ya wenye kubaki kwenye vitanda vyao. 
Wewe una hukumu ya wenye kubaki kwenye vitanda vyao. 
Haina maana usiache kitanda chako kamwe. 
Unahitajia wakati mwingine kutoka kitandani kwa haja fulani, hili haliathiri kukingwa kwako. 
Kinga bado iko pale pale Alhamdulillaah.
 
 
Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

No comments:

Post a Comment