Swali:
Ni
shaka ipi ambayo ni kufuru?
Je, shaka ya khiyari juu ya kuwepo kwa
Allaah (Ta´ala) au ukweli wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)…
Jibu:
Kuna
tofauti ya wasiwasi na shaka. Shaka haijuzu.
Pamoja na hivyo wasiwasi
unaweza kumjia mtu na akapambana nao kwa kumuomba Allaah kinga
kutokamana na Shaytwaan, akaupuuza na akanyamaza. Huu ndio wasiwasi.
Ama
shaka ni kufuru na ina maana ya mtu kuwa na kusita kati ya mambo
mawili; hajui kama ni hivo au sivyo; hajui kama aliyokuja nayo Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni sahihi au sio sahihi.
No comments:
Post a Comment