Sunday, April 24, 2016

UMUHIMU WA KUWATUNZA WAZAZI



بسم الله الرحمن الرحيم
إن الحمد لله، نحمده ونستعينه، ونستغفره، ونعوذ بالله من شرور أنفسنا، وسيئات أعمالنا، من يهده الله فلا مضل له، ومن يضلل فلا هادي له، وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمدا عبده ورسوله.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ] آل عمران:102   [يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا] النساء:1    [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾ يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا . الأحزاب:70-71
أما بعد،
فان أصدق الحديث كتاب الله، وأحسن الهدي هدي محمد، وشر الأمور محدثاتها، وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة، وكل ضلالة في النار

Hakika ametakasika yule ambaye amewajibisha na kuamrisha wema na kutimiza haqqi na kuiegemeza kwa kila anaestahiki na akawajibisha haki kwa wazazi wawili, na ikawa ni amri iliyoenea kwa walimwengu wote. Hakika ameamrisha ALLAH tabaaraka wata’la katika aya nyingi kuwafanyia wema na ihsani wazazi wawili.
Mfano wa kauli yake aliposema:

{وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلاَهُمَا فَلاَ تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلاَ تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلاً كَرِيماً* وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيراً} 
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.

Akaamrisha ALLAH tabaaraka wata’la ihsani kwa wazazi wawili katika namna zote za wema, nao ni katika kauli [unapozungumza nao] pale aliposema [basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima]. Vivyo hivyo kuwafanyia wema katika matendo; kimwili na kimali kwa kauli yake aliposema: (Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma).
Na akanyanyua ubora wanapofika katika hali ya uzee, kisha akakataza kuwavunjia adabu na kuwatusi, achilia mbali kuwaacha wakiteseka.

UWAJIBU WA KUWAFANYIA WEMA WAZAZI WAWILI.
Hakika ameamrisha Allah tabaaraka wata’la, na akawajibisha kwa njia ya wasia kuwafanyia wema wazazi wawili katika aya nyingi za qur’an. Pale ilipokuja amri ya wazi juu ya kuwatii, aliposema:
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَاناً
Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake wawili[1]
Ikaonesha wazi kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ni jambo la wajibu kwa kuwa ni wasia wa Allah kwetu. Bali akaliambatanisha jambo hilo la kuwafanyia wema wazazi wawili na twaa’ yake Allah tabaaraka wata’la pale aliposema:
وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mola wako mlezi ameamrisha kuwa msimuabudie yeyote isipokuwa yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema.[2]
Na kauli yake aliposema:
وَاعْبُدُواْ اللّهَ وَلاَ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئاً وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَاناً
Na mwabudieni Allah wala msimshirikishe na chochote, na muwafanyie wema wazazi wawili.[3]
Zikakusanya aya mbili hizi kuwa kufanyiwa wema wazazi wawili ni haqqi yao, bali akaifafanya haki hiyo kuwa ni ya pili baada ya tawheed yake Allah tabaaraka wata’la akionesha ukubwa wa jambo hilo [la kuwafanyia wema].
Amesema Al qurtwubiy [Allah amrehemu], kauli ya Allah “Na wazazi wawili kuwafanyia wema [ihsani]” maana yake ni:
برهما وحفظهما وصيانتهما وامتثال أوامرهما
Kuwafanyia wema na kuwahifadhi, kuwatunza na kutekeleza amri zao.
Katika kulisisitiza hilo, mpaka ikawa [wema kwa wazazi wawili] ni wenye kutangulizwa mbele hata kabla ya Sunnah za kujitolea kama vile Sunnah za kabla ya swala nk. Na kwa hili akaweka imamu muslim [Allah amrehemu] mlango katika swahih yake akiuita:
باب تقديم بر الوالدين على التطوع بالصلاة وغيرها
Mlango ambao unaelezea kutanguliza wema kwa wazazi wawili ni jambo bora kuliko swala za Sunnah na mengineyo (katika Sunnah za kujitolea)[4]
Kisha akataja kisa cha Jariyji Ar-raahib[5], akikielezea abu Hurairah [Allah amridhie] akisema:
وكان جريج رجلاً عابداً فاتخذ صومعة فكان فيها فأتته أمه وهو يصلي فقالت ياجريج فقال يارب أمي وصلاتي فأقبل على صلاته فانصرفت فلما كان من الغد أتته وهو يصلي فقالت : ياجريج , فقال : يارب أمي وصلاتي فاقبل على صلاته , فانصرفت , فلما كان من الغد أتته وهو يصلي , فقالت : ياجريج , فقال : أي رب أمي وصلاتي فاقبل على صلاته , فقالت : اللهم لاتمته حتى ينظر إلى وجوه المومسات ـ يعني الزانيات ـ فتذاكر بنو إسرائيل جريجاً وعبادته وكانت امرأة بغي يتمثل بحسنها فقالت إن شئتم لأفتننه لكم , قال : فتعرضت له فلم يلتفت إليها فأتت راعياً كان يأوي إلى صومعته فأمكنته من نفسها فوقع عليها فحملت فلما ولدت قالت : هو من جريج , فأتوه فأنزلوه وهدموا صومعته وجعلوا يضربونه , فقال : ما شأنكم , قالوا : زنيت بهذه البغي فولدت منك , فقال : أين الصبي فجاءوا به , فقال : دعوني حتى أصلي فلما انصرف أتى الصبي فطعن في بطنه , وقال : ياغلام من أبوك ؟ قال : فلان الراعي , فأقبلوا على جريج يقبلونه ويتمسحون به وقالوا : نبني لك صومعتك من ذهب, قال : لا أعيدوها من طين كما كانت ففعلوا .
. . . Na alikuwa Juraij mwenye kufanya ibada nyingi (mwenye taqwa), akajifanyia kijumba akawa (anafanya ibada) humo. Akamjilia mama yake (mzazi) na hali ya kuwa (Juraij) yu katika swala, akaita ((kumwita mwanae)): ((Ewe Juraij)), akasema Juraij: ((Ewe mola wangu, mama yangu [ananiita nikiwa katika] swala yangu)), akaendelea na swala yake, akaondoka (mama mzazi) na alipofika kesho yake akaja tena na hali yakuw Juraij yu katika swala, akaita: ((Ewe Juraij)), akasema Juraij: ((Ewe mola wangu, mama yangu [ananiita nikiwa katika] swala yangu)), akaendelea na swala yake, akasema (mama): ((Ewe Allah !usimfishe mpaka akutane na uso wa kahaba)). Zilienea khabari za Juraij na ibada zake kwa banu israeel. Na kulikuwa na mwanamke kahaba ambaye ni mzuri wa kiwiliwili akasema (kuwaambia watu): mkitaka nitamtia fitna (nitamhadaa Juraij na kumtia kwenye uovu): akajipeleka kwa Juraij, na Juraij hakumjali, akamwendea mchungaji ambaye alikuwa akiishi karibu na nyumba ya Juraij na akafanya naye uovu na akapata ujauzito, zama alipozaa akasema (yule mwanamke kuwaambia watu): huyu ni mtoto wa Juraij, watu wakamjia (Juraij) wakamtoa ndani, wakaivunja nyumba yake na wakaanza kumpiga. Akasema (Juraij): ((ni lipi jambo lenu?)) wakasema: ((umezini na kahaba huyu na ukakuzalia mtoto)) akasema: ((yupo wapi huyo mtoto?)) wakaja naye, akasema: ((niacheni niswali)) alipomaliza kuswali akamjilia mtoto akamminya tumboni na akamuuliza: ((Ewe kijana, ni nani baba yako?)) akasema (yule mtoto): ((fulani mchungaji)), wakamuelekea (watu) Juraij wakawa wakimkumbatia, wakimbusu na wakimgusa (wakikusudia baraka) na wakasema: ((tunajiandaa kukujengea nyumba yako kwa dhahabu)) akasema: ((hapana, ijengeni kwa mchanga kama mlivyoikuta mwanzo)).[6]

Tazama jinsi gani twaa’ ya mzazi ilivyokuwa ni jambo la thamani na lenye kheri na kuwaasi wao ni jambo la shari. Hakika wito wa mzazi ulikuwa bora zaidi kuliko swala za sunnah alizokuwa akiziswali kwani, mama alipoomba dua akalikubali Allah dua lake kwa dhati ya mzazi kwa mwanae. Kwani mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi ambayo ameihadithia abuu Hurairah [Allah amridhie] akisema:
(( ثلاث دعوات لا ترد : دعوة الوالد  لولده ، ودعوة الصائم ، ودعوة المسافر ))
Dua za watu watatu hazirudishwi: dua ya mzazi kwa mwanae, na dua ya aliyefunga, na dua ya msafiri.[7]

Na katika riwaya nyingine akisema:
(( ثلاث دعوات مستجابات لا شك فيهن ، دعوة الوالد على ولده ، ودعوة المسافر ، ودعوة المظلوم ))
Dua za watu watatu ni zenye kujibiwa: dua ya mzazi kwa mwanae, na dua ya msafir, na dua ya aliyedhulumiwa.[8]
Bali yatakiwa kuwapendelea wao na kuwatanguliza katika mambo yote ya kheri zaidi ya yeyote baada ya Allah na mtume wake,
Na yatosha uwajibu wa mtu kumhudumia mzazi wake kwa yale aliyoyataja mtume صلى الله عليه وسلم kwani,
سألت رسول الله صلى الله عليه وسلم : أي العمل أحب إلى الله ؟ قال : الصلاة على وقتها ، قلت : ثم أي ؟ قال : بر الوالدين ، قلت : ثم أي ؟ قال : الجهاد في سبيل الله "
Aliulizwa mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم : ni ipi a’amali inayopendwa Zaidi na Allah ? akasema: swala katika wakati wake, nikasema: kisha ipi? (Akasema): kuwafanyia wema wazazi wawili, nikasema: kisha ipi? Akasema: jihaad katika njia ya Allah.[9]
Akajaalia mtume صلى الله عليه وسلم wema kwa wazazi wawili ni bora zaidi kuliko jihadi katika njia ya Allah, na halikuwa hilo isipokuwa kutokana na ukubwa na uwajibu wake.



UJUMLA WA NAMNA ZA WEMA KWA WAZAZI NA MALIPO YAKE
Ndugu katika iyman, tambua kuwa wema kwa wazazi wawili ni katika njia ya mitume na Akalitaja jambo hilo Allah tabaaraka wata’la katika aya nyingi ndani ya qur’an. Kwalo akamsifia yahya [‘alayhis_salaam] akisema:
وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا
Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa Jabari muasi[10]
Na akamsifu pia kwalo jambo hilo ‘Iysa [‘alayhis_salaam] akisema:
وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا
Na nimtendee wema mama yangu, wala hakunifanya niwe jeuri, muovu[11]
Basi ikawa hakuna kufaulu wala kutengenekewa duniani na akhera isipokuwa kupitia kwao. Na likapata nguvu jambo hili kwa kauliya mtume صلى الله عليه وسلم kutoka kwa ibn ‘Abbas [Allah amridhie] akisema:
(( من أصبح مطيعاً لله في والديه أصبح له بابان مفتوحان من الجنة وإن كان واحداً فواحد، ومن أمسى عاصياً لله في والديه أصبح له بابان مفتوحان من النار، وإن كان واحداً فواحد، قال رجل : وإن ظلماه ؟ قال : (( وإن ظلماه، وإن ظلماه، وإن ظلماه )) .
Atakaepambaukiwa akiwa katika twaa’ ya Allah kwa wazazi wake atakuta milango miwili ya Jannah imefunguliwa kwa ajili yake, na ikiwa ni [mzazi] mmoja basi ni [mlango] mmoja, na atakayefikwa na jioni hali yakuwa amemuasi Allah kwa wazazi wake atakuta  milango miwili ya motoni imefunguliwa kwa ajili yake, , na ikiwa ni [mzazi] mmoja basi ni [mlango] mmoja, akasema mtu: hata kama atamdhulumu? Akasema: ((hata kama atamdhulumu, hata kama atamdhulumu, hata kama atamdhulumu)).

Na likatajwa jambo hilo hata ikawa kuwaasi wao ni katika madhambi makubwa yenye kuangamiza, kwani anasema mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi aliyoipokea Abu Bakrata [Allah amridhie]:
(ألا أنبئكم بأكبر الكبائر؟) ثلاثا قالوا: بلى يا رسول الله قال: (الإشراك بالله وعقوق الوالدين) وجلس وكان متكئا (ألا وقول الزور) ما زال يكررها حتى قلت ليته سكت
(Je, nikujulisheni [nikukhabarisheni kuhusu] madhambi makubwa kuliko yote?) (akayasema maneno haya mara tatu), wakasema (maswahaba): tujuze ewe mtume wa Allah! Akasema: (kumshirikisha Allah na kuwaasi wazazi wawili) kisha akaketi, [kanakwamba] ilikuwa somo limeisha, [kisha akasema] ([pia] na kiapo cha uongo) hakuacha kuwa akilikariri (akilirejerejea) hili mpaka nikajisemea (moyoni) laity angenyamaza[12]
Ikajulisha kuwa ni jambo lisilofaa kuwaasi na kuwahama wazazi, bali kumtusi ni jambo la muhali, tena lisilofaa zaidi kama alivyosema mtume صلى الله عليه وسلم katika riwaya nyingine akisema:
(( من أكبر الكبائر شتم الرجل والديه قالوا : يا رسول الله وهل يشتم الرجل والديه قال : (( نعم ، يسب أبا الرجل فيسب أباه ، ويسب أمه فيسب أمه ))
Miongoni mwa madhambi makubwa ni mtu kumtusi mzazi wake, wakasema (maswahaba): ewe mtume wa Allah! Na je mtu anamtusi mzazi wake? Akasema: ((ndio, anamtusi mtu baba wa mwenzie naye anamtusi babaye, na anamtusi mtu mama wa mwenzie naye anamtusi mamaye))[13]
Bali mtume صلى الله عليه وسلم akatangaza laana kwa yule mwenye kumlaani mzazi wake, akisema:
 (( لعن الله من لعن والديه)) [ صحيح الأدب المفرد ] .
Amemlaani Allah mwenye kumlaani wazazi wake[14]

Hata ikawa Jannah ni haramu kwa yule mwenye kuwaasi wazazi wawili pale aliposema mtume صلى الله عليه وسلم :
ثلاثة حرم الله تبارك وتعالى عليهم الجنة، مدمن الخمر، والعاق، والديوث الذي يقر الخبث في أهله
Watu wa namna tatu, Allah tabaaraka wata’ala ameharamisha juu yao [kuingia] Jannah, aliyekubuhu katika ulevi, na mwenye kuwaasi wazazi wawili, na duyuth[15] ambaye anaridhia uchafu katika familia yake([16]) [17]

Na akasema pia:
كل الذنوب يؤخر الله منها ما شاء إلى يوم القيامة إلا عقوق الوالدين، فإن الله يعجله لصاحبه في الحياة الدنيا قبل الممات
Madhambi yote huchelewesha Allah kutokana nayo madhambi hayo [kwa adhabu] vile atakavyo mpaka siku ya kiama isipokuwa kuwaasi wazazi wawili, hakika ya Allah humharakishia [adhabu] mwenye kuwaasi wazazi wake katika maisha ya dunia kabla ya mauti [yake][18]

Kwahiyo Allah tabaaraka wata’la akaweka makemeo makali kuhusiana na kuwafanyia ubaya na kuwaasi na kuwalaani wazazi wawili katika dalili hizo na zisizokuwa hizo katika hadithi zenye kutaja makemeo makali kwa mwenye kuwaasi wazazi wawili.
Kama hivyo ndivyo, basi tambua:
Hakika miongoni mwa wema kwa wazazi ni kuwalisha, kuwavisha na kuwanywesha, kadhalika kuzungumza nao maneno laini na kutowafanyia kibri, baba anahangaika usiku na mchana akitafuta cha kukulisha kama ambavyo mama anahangaika kumnyonyesha mwanae na zaidi ya hayo. Na miongoni mwa mambo mema ambayo kwayo Allah amewajibisha kuwafanyia wazazi ni kuwahurumia na kuwaombea dua.
Anasema Allah tabaaraka wata’la:
وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيراً
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.[19]

Tambua kuwa, kuwafanyia wema wazazi katika namna yoyote iwayo, ni sababu ya mtu kuiingia Jannah ya Allah tabaaraka wata’la. Hakika amehadithia Abu huraira [Allah amridhie], kutoka kwa mtume صلى الله عليه وسلم :
رغم أنفه، رغم أنفه، رغم أنفه، قيل: من يا رسول الله؟ قال من أدرك والديه عند الكبر أحدهما أو كليهما ثم لم يدخل الجنة
Imegota chini pua yake, imegota chini pua yake, imegota chini pua yake, pakasemwa: ni nani (huyo) ewe mtume wa Allah? Akasema: aliyewadiriki wazazi wake katika uzee, mmoja wao au wote wawili kisha hakuingia Jannah.[20]
Ikajulisha kuwa, kuwafanyiawema wazazi au mmoja kati yao ni katika sababu za mtu kuingia Jannah na kuepushwa na moto.
Na kuwafanyia wema ni katika sababu za kupata nusra ya Allah tabaaraka wata’la katika mabalaa, kama anavyohadithia mtume صلى الله عليه وسلم kutokana na hadithi ya watu watatu ambao walifunikwa na jiwe pangoni, pale aliposema mmoja wao:
 ( اللهم كان لي أبوان شيخان كبيران وكنت لا أغبق قبلهما أهلاً ولا مالا، فنأى بي طلب الشجر يوماً فلم أرح عليهما حتى ناما فحلبت لهما غبوقهما فوجدتهما نائمين فكرهت أن أوقظهما فلبثت والقدح على يدي انتظر استيقاظهما حتى برق الفجر فاستيقظا فشربا غبوقهما ، اللهم إن كنت فعلت ذلك ابتغاء وجهك ففرج عنا ما نحن فيه من هذه الصخرة ، فأنفرجت شيئاً.....)  

(Ewe Allah, nilikuwa mimi nina wazazi walio wazee, na nilikuwa siipi familia yangu maziwa kabla yao, siku moja, nilichelewa kurudi siku moja kwa bahati mbaya, nikafika nikiwa nimechelewa nao wakiwa wamekwisha lala, nilikamua maziwa kwa ajili yao ni nikawakuta wamelala, nikachukia kuwapa maziwa familia yangu kabla ya wao. Nikawasubiri na bakuli la maziwa li mkononi mwangu mpaka waamke hadi ikanikuta alfajiri, kisha wakaamka na wakanywa mziwa yao. Ewe allah ikiwa nilifanya kwa ajili yako basi tupe faraja sisi kutokana na hali tuliyonayo kutokana na jiwe hili, jiwe likasogea kidogo lakini hawakuweza kutoka)[21]

Kisha ikawa kuwafanyia wema wazazi wawili ni katika sababu za na kukunjuliwa rizki kwa ujumla wa kauli yake mtume صلى الله عليه وسلم aliposema:
من أحب أن يبسط له في رزقه وينسأ له في أثره فليصل رحمه
Yule anaetaka akunjuliwe katika rizki yake na kurefushwa umri wake basin a aunge undugu[22]
Na katika riwaya nyingine akasema:
من سره أن يمد له في عمره ويزاد في رزقه فليبر والديه وليصل رحمه
Yule anayetaka kuongezewa katika umri wake na azidishiwe katika rizki yake basi na amfanyie wema mzazi wake na aunge udugu[23]
Na zikawa radhi za Allah tabaaraka wata’la zi pamoja na radhi za wazazi kwa kauli ya mtume صلى الله عليه وسلم aliposema:
رضا الرب في رضا الوالد ، وسخط الرب في سخط الوالد
Radhi za Allah zi katika radhi za mzazi, na chuki ya Allah i- katika chuki ya mzazi[24]
Na katika riwaya nyingine
رضا الرب في رضا الوالدين و سخطه في سخطهما
Radhi za Allah zi katika radhi za wazazi wawili, na chuki ya Allah i- katika chuki yao[25]
Tazama ni ukubwa kiasi gani Allah tabaaraka wata’la akifadhilisha darja la wazazi mpaka kufikia kuwa humridhia mja maadamu mja huyo ameridhiwa na wazazi wake katika mipaka ya kisheria na humghadhibikia na kutokuwa radhi naye yule ambaye ameghadhibikiwa na wazzazi wake.

Bila ya shaka, hakika wema wa wazazi ni jambo kubwa na lenye fadhila nyingi hata na wizani wake ni wizani wa juu hata ikawa kuulipa wema wake huo ni jambo zito, kwani mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi iliyoihadithia Abu Huraira Allah amridhie amesema:
لا يجزي ولد والداً ، إلا أن يجده مملوكاً فيشتريه فيعتقه
 [Kamwe] mtoto haweza lipa wema kwa baba, isipokuwa atakapomkuta mtumwa, akamnunua akamwacha huru[26]

MIPAKA YA KISHERIA KATIKA KUWATII WAZAZI WAWILI
Hakika pamoja na kutajwa uwajibu wa kuwatii wazazi, pakatajwa pia kuwa twaa’ hiyo iwe ni katika wema na si uovu. Itakapokuwa amri ni katika kumuasi Allah tabaaraka wata’ala [iwe ni amri ya kulifanya jambo ovu au kuacha wajibu] hakika Allah tabaaraka wata’la ameikemea twaa’ hiyo pale aliposema:
{ وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ }
Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Lakini ishi nao kwa wema duniani, nawe ishike/ifuate njia ya anayeelekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu, name nitakujulisheni mliyokuwa mkiyatenda[27]

Allah akaamrisha kutowatii pamoja na daraja lao kwa mtoto wao, na hilo likatajwa kuwa ni miongoni mwa utimilifu wa imani ya mja, akisema:
لا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ أُوْلَئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ
Huwakuti watu wanaomuamini Allah na siku ya mwisho kuwa wanawapenda wanaompinga Allah na mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao au jamaa zao. Hao ameandikakatika nyoyo zao Imani, na akawapa nguvu kwa roho itokayo kwake[28]

Akasema pia:
 يَا أَيّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانكُمْ أَوْلِيَاء إِنْ اِسْتَحَبُّوا الْكُفْر عَلَى الْإِيمَان وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَأُولَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ
Enyi mlioamini ! msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanastahabu [wanapenda] ukafiri kuliko Imani. Na katika ninyi atakayewafanya kuwa ndio vipenzi vyake, basi ndio madhwaalim[29]

Na jambo hilo la kutomtii mzazi katika kumuasi Allah tabaaraka wata’la kwasababu yeye ni kiumbe, na kiumbe hana ukubwa wa kuzidi mipaka ya Allah tabaaraka wata’la: kama anavyosema mtume صلى الله عليه وسلم :
لا طَاعَةَ لأَحَدٍ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ , إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ
Hakuna twaa kwa yeyote katika kumuasi Allah, kwa hakika utiifu [kutii] ni katika mema[30]
Akasema pia:
لا طاعةَ لمخلوقٍ في معصية الخالق
Hakuna twaa kwa kiumbe katika kumuasi muumba[31]



KUJUZU KWANASIHI WAZAZI WANAPOKOSEA
Fahamu kuwa, Nasaha ni jambo ambalo limefanywa kuwa nguzo ya dini, ni juu ya mtoto kumnasihi babae kwa wema kama ilivyo juu ya mzazi kumnasihi mwanae atakapokengeuka katika mafundisho ya dini. Na hili ndio lililokaribu Zaidi na kufikia katika maisha ya furaha ya dunia na kuipata Jannah ya Allah tabaaraka wata’la.
Ansema mtume صلى الله عليه وسلم kupitia hadithi ya Tamiym Ad-darimy:
الدين النصيحة ، قلنا : لمن يا رسول الله ؟ قال : لله ، ولكتابه ، ولرسوله ، ولأئمة المسلمين وعامتهم
dini ni nasaha, tukasema kwa nani ewe mtume wa Allah? Kwa Allah, na kitabu chake, na mtume wake, na viongozi wa waislam na watu wote[32]

Fahamu kuwa nasaha kwa wazazi ndio njia mitume na waja wema waliotangulia katika zama za nyuma na zama hizi pia.
Anasema Allah tabaaraka wata’la:
 إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنْكَ شَيْئًا (*) يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا
Aliposema [Ibrahim a.s] kumwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini unaviabudu visivyo sikia, na visivyoona na visivyo kufaa kwa chochote? Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia elimu isiyokufikia wewe. Basi nifuate mimi, name nitakuongoza njia iliyo sawa[33]

Na Allah akaamrisha kushikamana na mila hii ya Ibrahiim [‘alayhis_salaam] akasema:
وَجَاهِدُوا فِي اللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ
Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Allah ukweli wa kufanya juhudi. Yeye amekuteueni. Wala hawakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim[34]

Na zisizokuwa hizo katika aya nyingi zenye kujulisha hilo. Na ikawa malipo yao kwa nasaha hizo ni Jannah, kama anavyosema Allah tabaaraka wata’la.

جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَنْ صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِمْ مِنْ كُلِّ بَابٍ
Jannah ya milele, wataiingia wao na walio wema miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na malaika wanawaingilia katika kila mlango[35]


NAFASI YA MAMA KWA BABA NA BABA KWA MAMA KATIKA WEMA
Hakika sharia ya dini imemtanguliza mama kabla ya baba katika wema na ikawa ni fadhwla za Allah tabaaraka wata’la kwa mama. Na hili ni kwa sababu ya udhaifu na unyonge wake katika kukabiliana na mambo. Hakika mama ndie ambae amekubeba tumboni mwake miezi tisa, akakuzaa kwa shida, akakunyonyesha, akakulea kwa huruma huku akikesha kwa homa zako na taabu zako, hudhikika yeye kwa dhiki zako kama ambavyo alikuwa akihangaika ili kuleta faraja yako.
Kwani anasema Allah tabaaraka wata’la:
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْناً عَلَى وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ
Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili, mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili (tukamuusia kuwa) nishukuru mimi na wazazi wako wawili, (na) kwangu ndio marejeo (yenu).[36]

Akasema pia:
وَوَصَّيْنَا الْإِنْسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا ۖ وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا ۚ
Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wakewawili. Mama yake amechukua mimba kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thelathini[37]
Anasema mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi ambayo ameihadithia Abu Hurairah akisema :
جاء رجل إلى رسول الله  فقال : يارسول الله، من أحق الناس بحسن صحابتي ؟ قال : ((أمك)) قال : ثم من ؟ قال : ((أمك)) قال : ثم من ؟ قال : ((أمك)) قال : ثم من ؟ قال : (( أبوك)).
Alikuja mtu kwa mtume wa Allah akasema: Ewe mtume wa Allah, ni nani (mtu) mwenye (kustahiki) haki Zaidi kwa wema wa usuhuba (wangu)? Akasema: ((mama yako)), akasema (tena yule mtu): kisha nani? Akasema: mama yako? akasema (tena yule mtu): kisha nani? Akasema: mama yako? akasema (tena yule mtu): kisha nani? Akasema: baba yako[38]
Na katika upokezi mwingine aliulizwa mtume صلى الله عليه وسلم  :
يارسول الله من أحق الناس بحسن الصحبة ؟ قال : (( أمك ثم أمك ثم أمك ثم أبوك ثم أدناك أدناك ))
Ewe mtume wa Allah ni nani mwenye haki zaidi miongoni mwa watu kwa kumfanyia wema wa usuhuba (kusuhubiana)? Akasema (mtume): ((mama yako, mama yako, mama yako kisha baba yako, kisha wa chini yako))

Ikawa haki ya wema kwa mama ni yenye kunyanyuliwa mara tatu dhidi ya haki ya baba, na hili ni kutokana na darja alilopewa na Allah tabaaraka wata’la na kufadhwilishwa kwake dhidi ya baba. Bali inasimuliwa Asmaa bint Abu bakr Allah amridhie:
قدمت على أمي وهي مشركة في عهد رسول الله  ، فاستفتيت رسول الله قلت : قدمت على أمي وهي راغبة ( طامعة عندي تسألني شيئاً ) أفأصل أمي ؟ قال : (( نعم صلي أمك ))
Alikuja kwangu mimi mama yangu katika zama za mtume s.a.w, na hali yakuwa ni mshirikina, nikamtaka fat_wa mtume wa Allah صلى الله عليه وسلم  nikasema kumwambia; amenijia mimi mama yangu na hali yakuwa akihitajia kutoka kwangu [nimsaidie shida yake] je, niendeleze uhusiano na mama [kwa kumsaidia shida yake]? Akasema: ndio endeleza uhusiano na mama yako[39]

Na hakulikubali hilo mtume صلى الله عليه وسلم  isipokuwa kwa ukubwa wa haki ya mzazi [hasa mama] kwa mwanae, isipokuwa ni kwa sababu ya unyonge na udhaifu wake. Kwani hakuna jambo lililokubwa zaidi kuliko kumtimizia mama haja yake anapokuwa na shida. hata akasema Ibn ‘Abbas [Allah amridhie]:
(( إني لا أعلم عملاً أقرب إلى الله عز وجل من بر الوالدة )).
Mimi siijui a’amali yenye kumkaribisha (mtendaji) kwa Allah mwenye ‘izza na utukufu kuliko kumfanyia wema mama[40]
Na akalifanya Allah jambo hilo kuwa ni katika sababu za mtu kusamehewa na kufutiwa madhambi yake. Kwani Amesimulia Abu bakr ibn Hafswa Allah amridhie kuwa, alikuja mtu kwa mtume صلى الله عليه وسلم  akasema:
يارسول الله إني أصبت ذنباً عظيماً ، فهل لي من توبة ؟ قال : هل لك من أم ؟ قال : لا ، قال : هل لك من خالة ؟ قال : نعم ، قال : فبرها ]
Ewe mtume wa Allah ! mimi nimefanya dhambi kubwa, je nina toba (ninaweza samehewa)? akasema (mtume): je, unaye mama? Akasema: hapana, akasema (mtume): je unaye shaangazi? Akasema: ndio, akasema (mtume): basi kamfanyiewema[41]

Na katika hadithi ya Al-baraa amesema mtume صلى الله عليه وسلم  :
[ الخالة بمنزلة الأم ]
Shangazi yu- katika daraja la mama[42]

Na kasha akakataza mtume صلى الله عليه وسلم juu ya kumuasi mama akimpwekesha kutokana na  baba akisema:

إن الله حرم عليكم عقوق الأمهات
Hakika Allah ameharamisha juu yenu kuwaasi wazazi wa kike [mama zetu].[43]

Tambua pia, pamoja na darja kubwa alilopewa mama dhidi ya baba, hakika mtume صلى الله عليه وسلم anasema:
الوالد أوسط أبواب الجنة
Baba ni mlango wa katikati (wa) Jannah([44])






HITIMISHO
Nimalizie kwa kusema; pale nilipopatia basi ni kwa uwezo wa Allah tabaaraka wata’la na pale nilipokosea basi mapungufu yanarudi kwangu kwa kuwa ni muhari kujinasibishia ukamilifu kwani ukamilifu ni wa Allah tabaaraka wata’la.

وصلى الله وسلم على نبينا محمد وعلى آله وصحبه أجمعين
Imekusanywa  na kuandikwa na
ABU HUDHEYFAH
Tahqiqy
ABU KHAYRAT
Nadhiru Ngozi



[1] Al-ahqaaf 15
[2]AL- Israa 23
[3] An-nisaa 36
[4] Sahih muslim
[5] Kupitia yeye mtoto mdogo alizungumza, na ikawa ni mmoja kati ya watoto watatu ambao walizungumza utotoni.
[6] Bukhari na muslim
[7] Sahihul jamii’, (sheikh Albany r.a)
[8] Sahihul jamii’, (sheikh Albany r.a)
[9] Bukhari na Muslim
[10] Maryam 14
[11] Maryam 32
[12] Imam Bukhari
[13] Bukhari na Muslim
[14] Sahih Muslim
[15] Duyuth ni mtu ambaye, uchafu unafanyika kwa watu wa nyumbani kwake miongoni mwa dada zake, wanawe na 
    mkewe lakini haongei wala hakemei bali anaona sawa tu 
[16] Na makusudio ni uchafu wa zinaa na mengineyo katika machafu.
[17] Imam Ahmad
[18] At-twabarany (Al_kabeer), Al-haakim (Al_awsatw), Imam Bukhari (Aadabul_mufrad)
[19]Al- Israa 24
[20] Bukhari na Muslim
[21] Bukhari na Muslim
[22] Bukhari na Muslim, imesimuliwa na Anas ibn Maalik.
[23] Bukhari na Muslim
[24] At-tirmidhy, silsilatus-swahih.
[25] At-twabarany
[26] Muslim
[27] Suratul_luqmaan 15.
[28] Suratul_mujaadillh 22
[29] Suratut_tawbah 23
[30] Bukhari na Muslim
[31] Imam Ahmad
[32] Bukhari na Muslim
[33] Surat Maryam 42-43
[34] Suratul hajj 78
[35] Suratur_raad 23
[36] Luqmaan 14
[37] Suratul Ah’qaaf 15
[38] Bukhari na Muslim
[39] Bukhari na Muslim
[40] Imam Bukhari [Aadabul_mufrad]
[41] Albaghwiy katika shirh sunnah
[42] Bukhari na Muslim
[43] Bukhari na Muslim, amehadithia hadithi hii ‘iysa al mughiyra Allah amridhie
[44] At-tirmidhy na Ibn Majah

No comments:

Post a Comment