Saturday, May 21, 2016

SHARTI LA MAZOEZI KWA MWANAMKE

Swali
Katika mji wetu wanawake wanakusanyika katika nyukumbi za mazoezi na wanacheza dufu na ngoma kwa lengo la mazoezi. Je, kitendo kama hichi kinajuzu?

Jibu
Mazoezi ambayo yana manufaa kwa mwili yanajuzu kwa sharti ikiwa wanawake wamejisitiri na hakuna wanaume wanaowaona. Katika hali hii mazoezi ni sawa. Lakini ikiwa yanaambatana na dufu na nyimbo, ni haramu. Kwa kuwa ni katika upuuzi wa haramu.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (01)
 http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh--14340126_0.mp3

No comments:

Post a Comment