Thursday, May 19, 2016

JE, INAJUZU KUMUULIZA SWALI KHATWIYB WAKATI WA KHUTBA?

Swali
Je, inajuzu kumuuliza swali Khatwiyb ilihali anatoa Khutbah siku ya Ijumaa?

Jibu
Kumuuliza swali la kielimu hakuna neno. 
Ama kumuuliza swali nje ya elimu katika mambo ya kidunia, hili halijuzu isipokuwa wakati wa dharurah. 
Kama mfano wa kisa cha yule aliyemuomba Mtume awaombee mvua. 
Hii ni dharurah, ni kitu cha dharurah.
 
Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

No comments:

Post a Comment