"إن
الحلال بين وإن الحرام بين"
عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُما
قَالَ : سمعتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:
(( إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ وَبَيْنَهُما أمورٌ
مُشْتَبِهَاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثيِرٌ مِنَ الناسِ،
فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ
فَقَد اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ في الشَّبُهاتِ وَقَعَ في
الْحَرَامِ، كالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ،
أَلا وَإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمىً أَلا وَإنَّ حِمَى الله مَحَارِمُه، أَلا وَإنَّ
في الجَسَدِ مُضْغَةً إذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ وإذَا فَسَدَتْ
فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلا وَهِيَ الْقَلْبُ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
HAKIKA HALALI IKO WAZI NA HARAMU IKO WAZI
Kutoka kwa Abu
Abdullah An-Nu’uman Ibn Bashiyr رضي الله عنه ambaye
alisema: Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema:
Halali iko wazi na
haramu iko wazi, baina yao ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi
hawajui. Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka anajisafisha
nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika
mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchunga anayechunga pembezoni
mwa mpaka, mara huingia ndani (ya shamba la mtu). Hakika kila
mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya Allaah سبحانه وتعالى ni makatazo Yake. Na hakika katika kiwiliwili kuna
kipande cha nyama kikitangamaa, kiwiliwili chote kitakua kizima, kikharibika
kiwiliwili chote huharibika. Basi jua (kipande hicho cha nyama) ni moyo.
Imesimuliwa na
Al-Bukhari na Muslim
CHANZO: Arbauna a-nnawawiy (No.6)
CHANZO: Arbauna a-nnawawiy (No.6)
No comments:
Post a Comment