Saturday, April 30, 2016

MWANAMKE KUONEKANA MIKONO YAKE NA SEHEMU YA NYWELE ZAKE

Swali:

Ni ipi hukumu ya mwanamke kuonesha sehemu katika nywele zake kwa kukusudia pamoja na kuvaa ´Abaa´ah na shungi? 
Je, kwa kufanya hivi anazingatiwa kuwa ni mwenye kufanya mapungufu katika Hijaab au ni mwenye kuonesha mapambo?
 

STARA YA MWANAMKE MBELE YA BINAMU YAKE WA KIUME

Swali:

Ni ipi hukumu ya mwanamke ambaye hakujisitiri kukaa peke yake nyumbani na ndugu yake mwanaume na binadamu yake ambaye kishabaleghe? Hoja yake ni kwamba wamekulia pamoja tokea utotoni.

JE, WAZINIFU WANA TAWBAH?

Swali:
Je wazinifu wana Tawbah?

 
Jibu
Kila mwenye madhambi ana Tawbah hata kafiri ana Tawbah.
قُل لِلَّذِينَ كَفَرُواْ إِن يَنتَهُواْ يُغَفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ
”Waambie wale waliokufuru: Wakikoma watasamehewa yaliyokwisha pita.” (8:38)

JE, KAFIRI AKIDHULUMIWA DUA YAKE HUPOKELEWA?

Swali:
Je Du´aa ya kafiri ambaye kadhulumiwa inakubaliwa?
 
Jibu
Ndio, inakubaliwa.

MASWAHABA WA MTUME MUHAMMAD ('aaleyhi ssalaam) NI BORA KULIKO WENGINE?

Swali:
Maswahabah ndio bora au al-Hawariyyuun?
 
Jibu

Maswahabah ndio bora. Kwa kuwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio bora kuliko Maswahabah wa Mitume wengine. Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu

Msimamo Kwa Wanawachuoni WAZUSHI

Msimamo Kwa Wanawachuoni WAZUSHI

Imaam Ibn Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:


"Hali kadhalika mzushi yuko dhidi ya Sunniy kwa sababu anamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na halinganishi Sunnah na maoni ya wanaume wala na kitu kingine kinachoenda kinyume nayo."

HUKMU YA PICHA

Swali1:
Ni ipi hukumu ya kuchukua picha za kumbukumbu sehemu takatifu?

Swali 2:
 Kwenye misikiti hii bila shaka kunakuwepo wanaume, wanawake na viumbe wengine na kuna uwezekano wakaingia ndani ya picha.

MAKHURAFI

Allaah Au Hawa Makhurafi?

Swali
Kwetu kuna baadhi ya Suufiyyah wanaosema kuwa maiti waliyomo ndani ya makaburi wanasikia du´aa na wanatumia dalili kwa hili kwamba inajuzu kuwaomba na kufanya Tawassul kupitia kwao...

Sunday, April 24, 2016

ADABU ZA KUISHI NA MKE



Huruma/Upole na Busara Kwa Mke Wako Unapotaka Kukutana Kinyumba

Inapendekezwa kuwa mtu anapotaka kufanya tendo la ndoa na mkewe katika siku ya kwanza ya ndoa, ambembeleze na amuonyeshe hali ya huruma na upole kama kumkaribisha kinywaji na kadhalika. Kama tunavyojifunza katika Hadiyth ya Asmaa bint Yaziyd ibn As-Sakaan ambaye alisema:

إني قَيَّنْتُ عائشة لرسول الله صلى الله عليه وسلّم، ثم جئته، فدعوته لجَلْوَتِهَا، فجاء فجلس إلى جنبها، فُاتي بعُسٍّ لينٍ، فشرب ثم ناوله النبي صلى الله عليه وسلّم فخفضت رأسها واستحيت، قالت أسماء: فانتهرتُها، وقلت لها: خذي من يد رسول الله صلى الله عليه وسلّم، قالت: فأخذت فشربت شيئاً، ثم قال لها النبي صلى الله عليه وسلّم: «أَعْطِي تِرْبَكِ» قالت أسماء: فقلت: يا رسول الله، بل خذه فاشرب منه، ثم ناولنيه من يدك، فأخذه فشرب منه ثم ناولنيه، قالت: فجلست ثم وضعته على ركبتي ثم طفقت أُديره وأُتبعه شَفَتِي لأصيب منه مَشْرَبَ النبي صلى الله عليه وسلّم، ثم قال لنسوة عندي: «نَاوِلِيْهِنَّ» فقلن: لا نشتهيه، فقال النبي صلى الله عليه وسلّم: «لا تَجْمَعْنَ جُوْعاً وكَذِباً»
"Nilimpamba ‘Aaishah kwa ajili ya Mjumbe wa Allaah, kisha nikamwita aje kumfunua na kumuangalia. Alikuja, akakaa pambizoni mwake, akaleta kikombe kikubwa cha maziwa ambayo alikunywa. Kisha akamkaribisha ‘Aaishah ambaye aliinamisha kichwa chake kwa kuona haya. Nikamgombeza na kumwambia: Pokea kutoka kwenye mikono ya Mtume Akachukua na kunywa kidogo. Kisha Mtume akamwambia: ((Wape mengine rafiki zako)) Hapo nilisema: Ewe Mjumbe wa Allaah bora chukua mwenyewe na kunywa na kisha unipe mimi kwa mikono yako. Akachukua na kunywa kidogo kisha akanipa mimi. Nikakaa chini na kuyaweka katika magoti yangu. Kisha nikaanza kukizungusha na kukifuatia kwa mdomo wangu ili nifikie pale alipokunywa Mtume. Kisha Mtume akasema kuhusu wanawake waliokuwepo pamoja na mimi: ((Wape wanywe)) Lakini wakasema: Hatuyataki (Yaani hawana njaa). Mtume akasema, ((Msichanganye njaa na uongo))[1][1]

UMUHIMU WA KUWATUNZA WAZAZI



بسم الله الرحمن الرحيم
إن الحمد لله، نحمده ونستعينه، ونستغفره، ونعوذ بالله من شرور أنفسنا، وسيئات أعمالنا، من يهده الله فلا مضل له، ومن يضلل فلا هادي له، وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمدا عبده ورسوله.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ] آل عمران:102   [يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا] النساء:1    [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾ يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا . الأحزاب:70-71
أما بعد،
فان أصدق الحديث كتاب الله، وأحسن الهدي هدي محمد، وشر الأمور محدثاتها، وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة، وكل ضلالة في النار

Hakika ametakasika yule ambaye amewajibisha na kuamrisha wema na kutimiza haqqi na kuiegemeza kwa kila anaestahiki na akawajibisha haki kwa wazazi wawili, na ikawa ni amri iliyoenea kwa walimwengu wote. Hakika ameamrisha ALLAH tabaaraka wata’la katika aya nyingi kuwafanyia wema na ihsani wazazi wawili.
Mfano wa kauli yake aliposema:

Vipi tuipokee Ramadhani SHEIKH QASIM MAFUTA (Hafidhwahullah)


Saturday, April 23, 2016

UZUSHI WAKATI WA KUOMBA DUA



KUFUKIZA UBANI WAKATI WA KUOMBA DUA
بسم الله الرحمن الرحيم
إن الحمد لله، نحمده ونستعينه، ونستغفره، ونعوذ بالله من شرور أنفسنا، وسيئات أعمالنا، من يهده الله فلا مضل له، ومن يضلل فلا هادي له، وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمدا عبده ورسوله.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ] آل عمران:102   [يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا] النساء:1    [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾ يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا . الأحزاب:70-71

Sifa zote njema anastahiki Allah aliyetukuka Mola mlezi wa walimwengu wote, swala na salamu zimshukie Kipenzi chetu mtume Muhammad (صلى الله عليه وسلم:) na maswahaba zake mpaka siku ya mwisho.

Friday, April 22, 2016

NASAHA KWA WANAWAKE



بِسمِ ٱلله الرَّحْمٰنِ الرَّحِيـمِ.

الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على رسول الله خاتم النبيين، وعلى آله وصحبه، ومن والاه إلى يوم الدين.
Ama baada ya kumhimidi Allah na kumtakia sala na salam mtume صلى الله عليه وسلم . Yapaswa utambue kuwa, hakika Allah tabaaraka wata’la aliumba kila kitu katika jinsi mbili na akamuumba mwanadamu katika jinsia hizo [mume na mke] kutokana na tone la manii baada ya kumuumba Adam kwa udongo uliovunda. Hakika zama zimepita na hakuna tofauti katika mwenendo wa Allah tabaaraka wata’la juu ya viumbe wake. Kwani ilipokuwa nafasi ya mwanadamu ni ya juu katika dini kuanzia mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, Allah tabaaraka wata’la aliusia utekelezaji wa maamrisho yake kwa wanaadamu na akawausia wanawake pia. Na alikua Mtume صلى الله عليه وسلم akiwausia kwa miongozo hiyo kwenye hotuba katika viwanja vya Arafat