Tuesday, May 7, 2019

ADABU ZA RAMADHANI
Kula Sahuwr (Daku)  

Imependekezwa kula sahuwr (daku) na hakuna madhambi kwa yule ambae hakufanya hivyo. Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: “Kuleni daku, kwani ndani yake kuna baraka” [Al-Bukhaariy na Muslim].

Sababu ni kuwa kula daku kunampa nguvu mwenye Swawm, kunamfanya awe mkakamavu, na kuifanya Swawm kuwa ni nyepesi kwake.