Thursday, September 6, 2018

JE, INAFAA KUTUNZA NGUO ZA MAITI ?

INAFAA KUTUNZA NGUO ZA MAITI ??  

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)



SWALI:

Je, inajuzu kuhifadhi nguo za maiti? Na ikiwa haijuzu, basi ni lilo bora kuzifanya?

EPUKA MAMBO HAYA EWE MUISLAM...!

بسم الله الرحمن الرحيم


Muhammad  Bin 'Abdil-Wahhaab Sulaymaan At-Tamiymiy

Jua ya kwamba mambo yanayomtoa Muislamu katika Uislamu ni mambo kumi:

Moja: 
Ni kumshirikisha Allaah Aliyetukuka katika ibada, Anasema Allaah:
“Hakika Allaah Haghufuri kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.  Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali.” (An-Nisaa: 116)
Na Anasema Allaah:
“Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni Motoni. Na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.” (Al-Maaidah: 72)
na miongoni mwa hizo shirki ni kuchinja kwa asiyekuwa Allaah kama anayechinja kwa ajili ya majini au makaburi.